GET /api/v0.1/hansard/entries/1060905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1060905,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1060905/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Sote tunakubaliana yakuwa hamna uchumi uliostawi katika nchi yoyote, isipokuwa bei ya mafuta iwebei iliyotulia. Bei zimetulia licha ya bidhaa kuzidi ama kupungua na wala sio masoko ya mafuta kuingiliwa na ujanja. Tunawasiwasi kwa sababu petroli na bidhaa zake zimepanda kwa bei haijawahi onekana katika nchi hii kwa muda wa miaka tisa. Leo lita moja ni takriban Ksh122. Ni aibu kwangu. Mwisho wa bei hii ulikuwa November 2011. Hii kupanda bei bila mipangilio imeadhili bei ya chakula, usafiri, utengenezaji wa bidhaa na bei ya kila kitu kwa jumla imepanda. Wakenya wanaumia na hawawezi kujimudu kimaisha. Wengi wanahisi ikiwemo walioko katika Jumba hili kuwa EPRA wameshindwa na jukumu lao kubwa zaidi kuifadhi Wakenya, licha ya sheria ya kenya kipengele 10(hh) ya Energy Act 2019 kuwapatia nyadhifa za kuweza kuwalinda Wakenya. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}