GET /api/v0.1/hansard/entries/1060906/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1060906,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1060906/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mvita, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Abdullswamad Nassir",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Bei kupanda zaidi za petroli ni vigezo ama parameters zinazotumiwa na EPRA ambazo hazieleki, hazikosawa na hazina mpangilio. Mpaka bei ya mafuta hapa Kenya iko juu na hailingani na bei za nchi zingeni katika dunia nzima. Ili Wakenya waweze kupunguziwa mizigo ya bei ya mafuta naomba uwelekezo wako kupitia kwa Kanuni za Kudumu za Bunge 218(2): (a) Kwanza, kamati hizi mbili zichunguze na kuingilia kwa undani EPRA kuangalia njia za kubadilisha viegezo vilivyowekwa na Energy (Petroleum Pricing) Regulations 2010 na the Energy, (Petroleum Pricing) (Amendment) Regulations 2012. (b) Ningeomba kwa unyenyekevu kwa niaba ya Wakenya wasizidi siku 30 waweze kurejea katika Bunge hili na kupeana ripoti yao ambayo itakuwa yenye kufahamika kwa watu wote. Asante sana, Mhe. Spika."
}