GET /api/v0.1/hansard/entries/1062083/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1062083,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1062083/?format=api",
    "text_counter": 595,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kwamboka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 9246,
        "legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
        "slug": "beatrice-kwamboka-makori"
    },
    "content": "ni wakati muhimu tuangalie maslahi ya wafanyi biashara wadogo; wawache kuchukua ushuru kwa hao wafanyikazi kwa sababu kazi zao zinafungwa mapema si kama kitambo. Bi. Spika wa Muda, ni wakati ambapo kamati zetu ambazo zitakuwa zikihudumu, kama Kamati ya Afya, wakati ambapo tunamwalika Waziri, ni lazima Waziri aelewe kuwa wakati huu ni wakati wa dharura. Lazima Wananchi washughulikiwe. Kwa hivyo, Waziri lazima afike mbele ya Kamati kujibu maswali ambazo wataulizwa. Wakati tunaenda mashinani, ningehimiza kuwa sisi Wabunge tuongee na wananchi wetu na tuwaeleze manufaa ya kupata chanjo hii. Pia, tukatiza mikutano ambayo tuko nayo katika maofisi. Bi. Spika wa Muda, naunga mkono huu mjadala wa kusitishwa kwa Bunge mpaka mwezi ujao. Asante sana, Bi. Spika wa Muda."
}