GET /api/v0.1/hansard/entries/106286/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 106286,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/106286/?format=api",
"text_counter": 317,
"type": "speech",
"speaker_name": "Ms. S. Abdalla",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 380,
"legal_name": "Shakila Abdalla",
"slug": "shakila-abdalla"
},
"content": "Asante Naibu Spika. Kwanza nataka kuchukua nafasi hii kumpongeza mhe. Affey kwa kuleta Mswada huu ili kipengele hiki cha Sheria kifutiliwe mbali. Bw. Naibu Spika, pia ningependa kuwaombea msamaha wale waliopitisha sheria kama hii hapa Bungeni. Mwenyezi Mungu awasamehe kwa sababu najua kwamba wale binadamu ambao wamedhulumiwa hawatawasamehe. Atakayewasamehe ni Mungu. Mungu awasamehe kwa sababu ni sheria ya dhuluma ambayo imedhulumu watu kwa miaka mingi. Nitashukuru sana ikiwa Bunge hili litafutilia mbali kifungu hiki cha sheria ambacho kitawapatia watu haki zao ambazo walikuwa wamedhulumiwa kwa muda mrefu. Bw. Naibu Spika, Tume ya Haki na Maridhiano ilipozuru sehemu kadhaa haikuweza kuwajibika kufanya shughuli zake kwa sababu ya kifungu hiki. Tume hiyo ililazimika kutofanya chochote. Iliambiwa na wananchi irudi ili ikafanye kazi ya kutoa hiki kifungu ama irudi kwa Wizara yake ijadiliane na Wizara hiyo ili hiki kifungu kiweze kutolewa. Tunasema kuwa Kenya ni nchi ya kidemokrasia. Lakini masikitiko ni kwamba hiyo demokrasia tunayosema iko Kenya bado haijakamilika ikiwa kifungu hiki kitaendelea kutumika kwenye nchi. Bw. Naibu Spika, maonevu ya mabavu ya maofisa wa Serikali bado yanaendelea katika sehemu zingine nchini. Kuna sehemu nyingi sana ambazo maofisa wanawadhulumu wananchi kimabavu kwa kuwaingilia nyumbani mwao na kuwashika kiholela kwa misako ambayo haina misingi na kuwadhulumu kwa kuwapeleka kortini na kupigwa faini kubwa kubwa. Mambo ya maonevu ya hali ya juu hufanyika kwa sababu kifungu hiki kinawapatia nguvu hawa maofisa kuendelea na dhuluma na maonevu kama hayo. Kwa hivyo, ningeomba ikiwa tutaweza kupitishia huu Mswada ili hii sheria ifutwe bila ya mahojiano marefu kwa sababu ni sheria ya dhuluma na wengi wamedhulumiwa. Wale waliopitisha hii sheria walifanya hivyo kwa maonevu ya kutaka kufanya dhambi zao. Walijua kwamba walikuwa wamefanya dhambi katika sehemu kadhaa za nchi na hawatataka dhambi hizo zijulikane wala watu waende kutetea haki zao. Kwa hivyo, tunaomba sheria hii ifutiliwe mbali na wale waliofanya dhambi hizo wapelekwe mahakamani ndio watu waweze kupata haki zao. Bw. Naibu Spika, kwa hayo machache, naunga mkono Mswada huu."
}