GET /api/v0.1/hansard/entries/106307/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 106307,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/106307/?format=api",
    "text_counter": 338,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Nashukuru, Bw. Naibu Spika, kwa nafasi hii, nami nichangie Mswada huu ambao ni wa maana sana. Nimewasikiza walionitangulia kuzungumza kwa makini na Mswada huu unafaa kuzungumziwa kwa nguvu zote. Bw. Naibu Spika, ni haki na ni ukweli kwamba katika nchi yetu ya Kenya tunapozidi kuzungumzia umoja wa Wakenya na kuweka nchi pamoja, matamshi au maneno yetu ni tofauti na matendo yetu. Tukiangalia kama kuna Mswada ulioweza kuletwa katika Bunge letu la kitaifa na nikaamua kwamba kutakuwa na ubaguzi wa haki, na utathibitishwa kwa kuandikwa chini--- Hata sio mazungumzo tu; watu watachukua kalamu, kuiweka wino na kuandika kwamba sehemu fulani, fulani katika nchi yetu tukufu ni sehemu ambazo hazitazingatiwa, na hazitaonekana kwamba zinakaa wananchi, au viumbe wa Mungu. Ati watu fulani watatengwa na sheria ya nchi, wawekwe kando na kusemekana kwamba katika taifa letu tukufu, mambo mabaya yakianza kupekuliwa, na kuchunguzwa, yawe ni ya jana au ya miaka kumi au miaka ishirini iliyopita, kuna sehemu fulani ambayo haitaweza kuangaliwa. Sisi kama wawakilishi wa wananchi, tunataka kusema kwamba ugandamizaji wa haki za Wakenya hauwezi kuendelea; waliopitisha Mswada huo walikosea sana! haifai tuishi katika makosa yaliyofanywa."
}