GET /api/v0.1/hansard/entries/106310/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 106310,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/106310/?format=api",
    "text_counter": 341,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "35 Thursday, 8th April, 2010(P) maridhiano ya Wakenya, haitaweza kuonekana kuwa ni ya haki; hii ndio sababu unaona kuna taharuki ya maneno na kasheshe; pahali popote inapojaribu kusimama, inaambiwa: “Hatuwaamini; ondokeni hapa!” Kwa sababu gani? Ukiangalia mauaji ya Wagalla yalivyotokea, hakuna kitu mpaka leo kinazungumziwa! Maisha ya binadamu mbele ya macho ya Mwenyezi Mungu ni sawa. Kwa hivyo, namuunga mkono Balozi Affey kwa kuleta Mswada huu katika Bunge ili tuweze kuuzungumzia na kuupitisha kwa kauli moja. Tunasema kwamba sio tu baada ya kuunyakua Uhuru ndio tutaangalia madhambi ya Wakenya. Tutaangalia hata madhambi yaliyotendewa Wakenya na wakoloni; hii ndio sababu sasa unasikia kuna kesi tunafanya Uingereza ya Mau Mau na wananchi wa Kenya waliosulubishwa na Mwingereza. Itakuwaje sisi tumweke Mwingereza hapa, tumshurutishe kulipa ridhaa kwa Wakenya halafu turuke makosa yaliotendeka zamani, tuje tena tuanze kuchunguza ya juzi, ilihali hapa katikati kuna wengine tunaotaka kuwazika wakiwa hai na kuwalazimisha kusahau haki zao? Nataka kusema kwamba, kama tunaanza na Mwingereza vile tumeanza, ili tuonekane tuna usawa, na ili tuangalie viumbe wa Mungu waliogandamizwa katika sehemu za Lamu, Wajir na sehemu zingine zote, mpaka Marsabit na Mkoa wa Kaskazini katika nchi yetu tukufu---. Ili tuonekane tunabadilika katika uongozi wetu, na tunasahau ubaguzi katika maisha ya binadamu na kusema kwamba yaliyotokea zamani sio tu tusahau--- Kama tunasahau, tusahau kila kitu hata yaliyotokea jana au leo asubuhi! Lakini kama ya asubuhi hatusahau, basi hata ya miaka 20, 30 au 40, hatuwezi kusahau; tutadai na kusema kwamba haki iwekwe katika uwazi ili wananchi wa Kenya waweze kuelewa ni kitu gani kilichotokea. Nimesikia, na ni aibu – na sitakubali kamwe - wananchi fulani wakitoka sehemu zao kuja hapa Nairobi, wanaambiwa: “Mkifika Kenya, wasalimieni Wakenya.”"
}