GET /api/v0.1/hansard/entries/1063105/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1063105,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1063105/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Jambo la mwisho ni kumshauri kuwa marehemu Sen. Haji alikuwa na jukumu la kitaifa. Aliweza kuhudumu Serikalini katika nyanja mbalimbali na alitegemewa na wengi kusimamia maswala mazito ya usalama katika Seneti. Hata alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Pili katika Kamati ya BBI ilikuwa ni jukumu lake kubwa sana. Hii iliiona kama nafasi ya kuwaunganisha Wakenya. Unapochukua majukumu yako ndugu Sen. Haji Abdulkadir Mohamed ni lazima ufuatilie kwa makini na ufuate nyayo za mzee kuhakikisha malengo aliyoyasimamia hayawezi kutofautiana na malengo yako binafsi."
}