GET /api/v0.1/hansard/entries/1063128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1063128,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1063128/?format=api",
    "text_counter": 120,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Shukran, Bw. Spika. Kwanza ningependa kutoa kongole kwa niaba yangu na ya watu wa kaunti ya Kilifi kwa ndugu yangu, Sen. Abdulkadir Haji, hususan watu wa Garissa kwa kumchagua Sen. Abdulkadir Haji kama Seneta wa Garissa bila upinzani wa aina yoyote. Sen. Abdulkadir Haji ni kitinda mimba wa Seneti. Kawaida ya sisi watu wa Pwani na Wakenya kwa jumla, huwa tunasema kwamba kitinda mimba ni mtoto wa mwisho anayependwa na kila mtu. Ninahakika kwamba tumeshaona vile watu wamekupokea katika Seneti na wamekua na imani na upendo kwako. Usibwage morale ya watu wa Garisaa kama Seneta wao. Wapee heshima vile Sen. Haji aliwapea heshima. Pili, Abdulkadir Haji si jina geni katika Kenya; alionyesha umaarufu wakati Kenya ilipigwa na magaidi kwa kitendo cha kumtetea na kumbeba mtoto mchanga ambaye aliahidiwa kuwa ana miaka mingi ya kuishi. Ni kitendo ambacho kilivunja roho za Wakenya wote. Wakenya wote walimpenda kwa ukakamavu wake na ujasiri alio nao. Mimi binafsi ninasema kwamba yeye ni shujaa na Seneta wetu. Karibu sana katika Jumba la Seneti. Hili ni jumba ambalo atajifundisha mengi. Ataketi na waheshimiwa ambao wamekua na experience kubwa sana kama Sen. Haji. Sen. Abdulkadir Haji ataweza kujifundisha na nina hakika kuwa atafaulu katika njia zake zote za kutekeleza kazi yake kama Seneta. Isitoshe, watu wa Garisaa hawakukosea hata kidogo. Walionyesha msimamo na matumaini. Wazee wa kule Garisaa wakiketi na kumwomba Mungu ampe ndugu yetu maisha marefu, ushujaa utaendelea kuonekana, na watu wa Garisaa watapata usaidizi. Vile Sen. Haji alikua anawapatia matumaini, ndivyo yeye pia atawapea. Bw. Spika, ukiniruhusu kumalizia, kwa Waislamu wote, kama vile ndugu yetu aliyekuja katika Seneti, huu ni mwezi mtukufu. Mwezi utaanza kesho na Waislamu wote katika Kenya watakua wakifunga katika huu mwezi mtukufu. Mimi nawatakia kila la heri Waislamu wote walio Kenya. Wawe na mwezi mtutkufu wa Ramadhan na Mwenyezi Mungu awe pamoja nao. Shukran, Bw. Spika."
}