GET /api/v0.1/hansard/entries/1063344/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1063344,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1063344/?format=api",
"text_counter": 336,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, hii Ripoti inasema kwamba Serikali isicheleweshe hizi pesa kwenda kwa Serikali za ugatuzi. Hizi pesa zinahitajika kupeleka madawa, maendeleo na vitu vingi ambavyo vinaweza kurahisisha maisha ya watu wa kaunti kuwa bora zaidi. Pesa hizi zina maana sana. Vile vile, ningependa kutoa onyo kwamba wote ambao wanahusika kuangalia hizi pesa wazitumie kwa usawa; zisitumiwe ovyo au kwa njia ya ufisadi. Hizi pesa ni muhimu kuleta miradi mbali mbali katika serikali za kaunti. Kupitia serikali za ugatuzi, barabara zinatengenezwa, hospitali zinapata dawa, na kina mama wanapata njia ya kwenda kwa shughuli zao mbali mbali. Hizo shughuli zote zinategemea hizi pesa. Bi. Spika wa Muda, la mwisho, ni lazima kuwe na mahospitali. Naona muda wangu umekwisha, lakini hivi juzi kumekua na ajali katika barabara ya Malindi. Kumekua na ajali mbali mbali---"
}