GET /api/v0.1/hansard/entries/1063350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1063350,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1063350/?format=api",
    "text_counter": 342,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuchangia Mswada wa ugawaji wa rasilimali katika Muhula wa 2020/2021. Kwanza, ningependa kujiunga na wenzangu ambao wamezungumzwa kabla yangu wakichangia Mswada huu. Ninaunga mkono Mswada huu. Donda sugu ambalo liko katika nchi yetu hivi sasa ni ufisadi. Ufisadi umetanda katika kila sehemu ya Serikali, iwe ni serikali za ugatuzi au Serikali Kuu. Hii ilidhibitishwa na Rais Uhuru Kenyatta hivi majuzi aliposema kwamba kwa siku moja, Kshs1 billioni zinapotea kwa sababu ya ufisadi. Kwa hivyo, Sisi kama Seneti, katika jukumu letu la kuchunguza na kuangalia Serikali, inafaa tufanye mambo zaidi kuliko tunavyofanya sasa. Bi. Spika wa Muda, hivi majuzi Mombasa kulizinduliwa daraja la watu kuvuka kwa miguu kutoka upande wa Likoni kuingia mjini. Daraja hili limesababisha watu kuzuiliwa kuvuka kutumia ferry kati ya Saa Kumi na Moja alfajiri hadi saa mbili asubuhi, na Saa Kumi jioni mpaka Saa Mbili usiku. Hii imesababisha msongamano mkubwa katika daraja lile. Daraja hilo halijachunguzwa na kudhibitiwa kuwa lina uwezo wa kubeba watu wangapi kwa wakati mmoja. Wale wanaovuka kwa sasa ni wengi sana kwa sababu kumekua na uhaba wa vyombo vya usafiri kutoka Likoni kwenda mjini. Kwa hivyo, lengo la kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona halitaweza kufikiwa kwa sasa kwa sababu watu wanasongamana. Vile vile, hawana nafasi ya kutembea vile walivyokua wanatembea awali. Tatizo lingine lilochangiwa na hili daraja ni biashara, hususan meli zinazoingia kushusha na kupakia mizigo katika Bandari ya Mombasa. Kazi yao imekatizwa. Kati ya Saa Kumi na Moja alfajiri mpaka Saa Mbili asubuhi, meli zile haziwezi kuingia ndani ya bandari ili kushusha mizigo. Vile vile, inapofika Saa Kumi jioni, meli haziwezi kutoka nje ya Bandari ya Mombasa. Hii inasababisha msongamano wa meli katika Bandari la Mombasa na pia inaweza kusababisha meli zinazoingia Bandari ya Mombasa zilipishwe gharama zaidi kwa sababu kila meli ina wakati wake wa kusafiri."
}