GET /api/v0.1/hansard/entries/1063377/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1063377,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1063377/?format=api",
"text_counter": 369,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Loitiptip",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13512,
"legal_name": "Anuar Loitiptip",
"slug": "anwar-loitiptip"
},
"content": "Kwa sababu ya muda, nitazungumza maswala mawili tu. Swala la kwanza ni kuhusu ufisadi. Zote tunajua kuwa kazi ya Bunge la Seneti ni kusimamia rasilimali za kaunti na kuweza kuhakikisha kuwa rasilimali zimefika katika Kaunti. Lakini, bado kuna ufisadi na viongozi wetu wamedhibiti ya kwamba Kshs2 bilioni zinapotea katika hii nchi kila siku na hiyo ni hali ya kusikitisha. Ningependa hii iwe changamoto kwa wale viongozi ambao wako mashinani, wakiongozwa na magavana. Hao viongozi wanafaa kujua ya kwamba rasilimali ambayo tumependekeza iwafikie mashinani ni pesa za wananchi, kwa hivyo wazitumie vizuri."
}