GET /api/v0.1/hansard/entries/1065481/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1065481,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1065481/?format=api",
"text_counter": 110,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Aisha Jumwa",
"speaker": {
"id": 691,
"legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
"slug": "aisha-jumwa-katana"
},
"content": " Asante. Kuhusu Mswada ambao ulipelekwa katika mabunge yetu ya kaunti, tulipata kujua kwamba Mwenyekiti wa IEBC alipata copy moja, ikawa gazetted. Lakini zile ambazo zilipelekwa katika County Assemblies kuzungumziwa zilitoka katika Secretariat ya BBI. Zilipofika kwa Mwenyekiti, Bw. Chebukati, hazikuwa Bills ambazo zimekuwa gazetted. Mimi nataka niseme hilo peke yake linamaanisha kwamba tayari sheria ilikuwa imehujumiwa. Hii ni kwa sababu zile Bills ambazo zilipelekwa kule katika mabunge yetu ya kaunti nyingine zilikuwa sawa ilhali nyingine hazikuwa sawa. Kwa sababu hiyo, mimi napinga. Hatujui hata leo tukipitisha huu Mswada kama Bunge la taifa kama kuna ukweli kwamba Mswada huo tumeupitisha ndio utapelekwa katika referendum yaani kura ya maoni. Inaonekana kuna Miswada mingi maana kila leo inatolewa hii kesho inatolewa ile. Kwa sababu hiyo hakuna uaminifu katika mchakato mzima huu wa BBI. Jambo ambalo limenistaajabisha si kwamba eti tumevunja sheria kama Bunge. Lakini ni jambo la aibu kwamba kikao cha dharura ama kikao hususan, kinaweza kuitwa ili Wabunge wakatize muhula wao wa mapumziko kuja kuzungumzia mchakato wa BBI badala ya kuzungumzia matatizo yanayo mwathiri mwananchi katika hali hii ngumu ya maisha katika nchi yetu hii ya Kenya. Tungekuwa leo tunazungumzia angalau ripoti ya kutoka kwa wizara ya Afya na mchakato mzima ambao serikali yetu kupitia Mheshimiwa Uhuru Kenyatta imeweka kumhusu mwananchi. Lakini leo tunazungumzia..."
}