GET /api/v0.1/hansard/entries/1065489/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1065489,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1065489/?format=api",
"text_counter": 118,
"type": "speech",
"speaker_name": "Malindi, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Aisha Jumwa",
"speaker": {
"id": 691,
"legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
"slug": "aisha-jumwa-katana"
},
"content": "mzigo wa kutulipa mishahara sisi Wabunge 416. Tunazungumzia kumwongezea mzigo wa 650 wa Wabunge. Wabunge tunaupata mshahara wetu kikamilifu. Lakini walioko kule nje wanaumia. Ukiangalia biashara ya utalii na Transport Industry, utapata watu ambao wamefinyiliwa. Sekta nyingi za watu ambao wanafanya biashara katika nchi hii ya Kenya zimeumia. Ni mikakati gani ambayo sisi kama Bunge ama kama taifa, kwa niaba ya mwananchi wa chini, tumeweka? Ukiangalia hakuna. Bibilia inasema katika Kitabu cha Mathayo 6:33 kwamba tuutafute ufalme wa mbinguni na vyote tutaongezewa. Lakini katika taifa la Kenya, tunasikia kwamba tutafute BBI na mizigo yote tutaongezewa. Tutaongezewa ushuru kwa sababu ya kuwalipa Wabunge 650. Tutaongezewa mizigo ya kodi. Ni jambo la kusikitisha sana. Tunapokaa hapa Waheshimiwa, nawaomba tufikirie mwananchi kwanza. Mimi naamini kwamba hakuna aliyesema anahitaji Wabunge 650 katika Bunge la Kumi na Tatu linalokuja. Ndio maana tunasema Mswada huu au Ripoti hii ni ya kukataliwa. Ninaamini Wananchi kule nje wananiona. Tukipitisha, watakaoumia ni wananchi. Sisi tutakuwa starehe hapa hata kama tuko mia saba na watatulipa. Kwa hivyo, mimi nataka niseme kuwa wananchi kule nje wajipange na wajue kwamba huu ni mzigo wao. Sio mzigo wa Wabumge ambao wamekaa starehe ndani ya Bunge hili letu la taifa."
}