GET /api/v0.1/hansard/entries/1065619/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1065619,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1065619/?format=api",
    "text_counter": 86,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi hii ili na mimi nichangie katika huu Mswada muhimu sana katika historia ya nchi yetu. Nilikuwa nimepanga hapo awali kuchangia Mswada huu kwa lugha ya Kingereza kwa sababu nilikuwa mmoja wa Wanachama katika Kamati. Tuliangazia masuala mengi ambayo yana utata na ambayo yametajwa ndani ya Bunge. Lakini kwa sababu kuna Waheshimiwa wenzangu waliokuja hapo awali kuzungumza mambo ambayo mengine yalikuwa si ya kweli, nimeona ni muhimu kuzungumza na kutoa mchango wangu kwa lugha ya Kiswahili. Hii ni kuhakikisha Wapwani, watakapoamua kupigia kura Mswada huu katika kura ya maoni, basi watapigia kura wakijua ukweli halisi wa mambo. Nataka kusema kutoka mwanzo kuwa naunga Mswada huu mkono, kisha naunga sana. Nami pia nataka kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Raila Amollo Odinga ambaye ni kinara wa chama changu na aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hii. Pia namshukuru Rais Uhuru Kenyatta mwanzo kwa Handshake na kuibua hii sheria ya BBI. Kwa kweli, imeleta mambo mazuri sana ambayo yatatusaidia kupunguza kutengwa kwa sehemu nyingi za nchi hii. Ningependa pia kujulisha Bunge hili jambo. Kama nilivyosema awali, nilikuwa Mwanachama katika Kamati ya JLAC iliyojadili na kuleta Ripoti hii. Ningependa kushukuru kila mmoja aliyechangia Ripoti hii hadi ikawa nzuri ilivyo. Kamati hii ilipoongozwa na Wenyekiti wetu wawili wa Bunge la Taifa na Seneti, iliangalia masuala tofauti tofauti kwa upana na urefu. Mimi ni mmoja ya Wanakamati waliotia sahihi ile Ripoti ndogo iliyoangazia masuala ya kuwa na maeneo Bunge 70 mapya. Nimesema toka hapo awali katika Kamati yangu, tulikubaliana kuwa kipengele chochote katika Mswada ambacho kinapinga Katiba kikipitishwa katika kura ya maoni, kipengele hicho kinakuwa halali kwa Katiba. Kwa hivyo, sikukubaliana na wenzangu katika Kamati waliosema kuwa Sehemu ya Pili sio ya kikatiba. Kama Kamati, tulikubaliana kuwa kipengele chochote ambacho ni kinyume na Katiba kikipitishwa na wananchi kinakuwa Katiba. Hivi sasa sikubaliani kuwa sehemu ya Mswada yenye kuorodhesha maeneo bunge 70 ni kinyume cha Katiba. Sehemu 257 ya Katiba yetu inatoa ruhusa kwa Mkenya yeyote kuleta kipengele kubadilisha Katiba. Kama ilivyoashiriwa jana na Kiongozi wa Walio Wachache, mwananchi yeyote anaweza kuleta kipengele cha kuondoa Bunge au Mahakama humu nchini au kupendekeza mfumo tofauti kabisa na ule ambao tunao. Iwapo Katiba inamruhusu mtu yeyote kuleta kipengele hicho, kwa nini isiwe kipengele cha kuongeza maeneo bunge? Kuna baadhi ambao walitaka kuja Bungeni kusema tuibadilishe sehemu hii ya Mswada. Kama Kamati tumezungumza na naona kuwa umekubali kuwa hatuwezi kubadilisha sehemu yeyote ya Mswada huu. Kuna njia mbili tu ya kubadilisha Katiba ya sasa: Kupitia Bunge na kupitia Wakenya. Katika Mswada huu, tumesahau zaidi ya watu milioni tatu waliotia sahihi na nina uhakika kuwa waliunga mkono kwa sababu ya orodha ya maeneo 70 na tutakuwa tunakiuka haki zao za kikatiba kuwaambia kuwa Mswada huu hauwezi kuwa kwenye Katiba. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}