GET /api/v0.1/hansard/entries/1065620/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1065620,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1065620/?format=api",
    "text_counter": 87,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Kuna watu wanaouangalia Mswada huu kama umeletwa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mheshimiwa Raila Odinga na Mhe. Uhuru Kenyatta lakini kama nilivyosema hapo awali kuna njia mbili tu ya kubadilisha Katiba. Hao pia wana haki kama Mkenya mwingine kubadilisha Katiba iwapo wanataka hivyo kwa sababu ni Wakenya na wanapiga kura. Mhe. Millie Odhiambo alikuuliza jana maoni yako kama Spika; je katika haki za hii nchi, kuna Mkenya ambaye ana haki zaidi kuliko mwenzake? Nina uhakika utatuambia kuwa kila Mkenya ana haki sawa, ikiwa ni Mkenya wa kawaida au Rais wa nchi hii."
}