GET /api/v0.1/hansard/entries/1065621/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1065621,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1065621/?format=api",
    "text_counter": 88,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Nikiongeza maoni mengine, Sehemu 50 ya Mswada huu inasema kuwa kaunti zetu zitaongezewa fedha kutoka asilimia 15 mpaka 35. Hili ni jambo nzuri kwa sababu kutoka mwaka 2013 tulipoanza ugatuzi, kaunti zimekuwa tu na asilimia 15. Wananchi wengi wameona faida na tofauti ya uongozi wa ugatuzi na uongozi wa Serikali ya juu. Iwapo mabadiliko yamekuja licha ya changamoto tofauti tofauti na asilimia 15, je asimilia 35 itaweza kuleta mabadiliko ya aina gani katika hii nchi? Kuna wale ambao wana propaganda na wanataka kuupinga Mswada huu kwa sababu zao na wanatatiza wananchi kwa kuwaambia iwapo Serikali inashindwa kutuma aslimilia 15 kwa kaunti, je itaweza kutuma asilimia 35? Hii ni hesabu rahisi sana na inaweza hata kufunzwa kwa shule ya chekechea. Inafananishwa na kibakuli chako cha senti. Ukiangalia kikapu cha nchi cha pesa, zile pesa zinazopatikana na nchi kwa mwaka huu, asilimia 15 hivi sasa zinaenda kwa serikali za kaunti, kwa hivyo iwapo Serikali itapata bilioni moja, trilioni au shilingi mia, lazima asilimia 15 iende kwa serikali za kaunti. Kwa hivyo kusema asilimia 35 ni kusema kuwa ule mfuko wa kila mwaka ndio utagawanywa na asilimia 35 lazima ziende mashinani. Serikali za Kaunti zinalalamika kuwa pesa zao zinacheleweshwa lakini mwisho wa siku zinafika kwa sababu ya Kipengele hiki kwenye Katiba. Siku nyingi tumelalamika kuwa pesa zinakaa Nairobi au zinashughulikia watu katika sehemu zingine za nchi lakini sasa pesa zitaongezwa mashinani ili wananchi wafaidike na serikali yao iliyo karibu. Mimi hushangaa na wananchi katika mitandao na sehemu za mazungumzo wanaopinga Mswada huu ijapokuwa si wengi. Kama nilivyosema awali, Mswada huu utaleta manufaa mashinani. Mhe. Spika, kitu kingine ni kuwa maeneo bunge sabini mapya yameongezwa. Ni muhimu kwa Wapwani kujua kuwa bila BBI, kuna maeneo bunge kumi ambayo hayatakuwa tena baada ya mwaka 2022 tukienda kupiga kura kwa sababu ya Katiba ya sasa. Wananchi katika maeneo hayo hawatoshelezi kwa hivyo ni lazima IEBC iweze kufuta maeneo hayo kumi. Maeneo hayo kumi yako Lamu, Tana River, Taita Taveta na Matuga kule Kwale. Kwa hivyo, BBI itasaidia maeneo hayo Pwani yasifutwe na kutuongezea mengine kumi. Sio tu kwa upendeleo bali ni haki yetu ya miaka mingi kulingana na idadi ya watu. Maeneo manne yataenda Kilifi, tatu yaende Mombasa, na tatu yatapewa Kwale ninakotoka. Nataka kuwasihi Wapwani kwa hilo waunge BBI mkono iwapo kura ya maoni itakuja mashinani. Ningependa kumwambia Mbunge wa Malindi aliyepinga Mswada huu abadilishe maoni yake na kurudi nyuma na kuunga mkono kwa sababu Kaunti yake ya Kilifi itapata maeneo bunge manne ambayo itawapa wananchi uwakilishi mwingi zaidi, CDF, basari, ujenzi wa barabara, masuala ya kujenga mashule na kuhakikisha kuwa shule zetu zina vifaa vya sayansi ambavyo hivi sasa hazina. Ningependa pia kuangazia masuala ya jinsia. Kwa mara ya kwanza huenda kama Wakenya tukawa viongozi ulimwengu mzima kwa kusawazisha masuala ya jinsia. Baada ya kushindwa kuleta usawa hapa Bungeni, BBI italeta usawa ya sheria ya theluthi mbili ya jinsia katika Bunge letu la kitaifa. Hapo awali, Katiba ilikuwa imetengeneza sheria kusaidia Seneti na pia ilisaidia serikali za kaunti kutimiza masharti ya theluthi mbili. Lakini wale waliotunga Katiba mwaka wa 2010 The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}