GET /api/v0.1/hansard/entries/1065622/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1065622,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1065622/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kwale CWR, ODM",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Zuleikha Hassan",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "walisahau kutuwekea kipengele cha kusawazisha jinsia hapa Bunge la Taifa. Th e Building BridgesIntitiative (BBI) inaleta hicho kipengele na hiyo shida itaisha. Tutakuwa nusu kwa nusu kijinsia katika Seneti. Wananchi katika kila kaunti watachagua maseneta wawili, mmoja wa kike na mmoja wa kiume. Hili ni jambo kubwa sana duniani. Hata nchi zinazoongoza kidemokrasia wameshindwa kufikia kiwango hiki. Jambo lingine ni katika viti vya gavana na naibu gavana. Italazimu kama gavana ni mwanaume, mdogo wake atakuwa mwanamke; kama gavana ni mwanamke, mdogo wake atakuwa mwanaume. Hiyo pia italeta nusu kwa nusu ya uwakilishi wa kijinsia. Haya ni mambo muhimu sana ya maendeleo. Wengi huuliza kwa nini ni vizuri kuwe na usawa wa kijinsia. Nikiwa Kwale napenda kuelezea wananchi hivi: ni mfano wa shughuli za nyumbani kama harusi au mazishi. Je, katika familia unaweza kufanya harusi, shughuli ndogo tu, ifaulu na wanawake peke yao au na wanaume peke yao? Jibu mara nyingi ni kuwa haiwezekani ama ikifanyika shughuli haitafana. Huo ndio umuhimu wake. Wengine wamesema kwamba kuwa na Wabunge zaidi utakuwa mzigo kwa taifa. Huo sio ukweli. Mzigo mkubwa Kenya yetu ni ufisadi ambao unakula theluthi mbili za pesa zetu za bajeti ya mwaka nzima. Bunge linatumia asilimia moja peke yake ya bajeti ya taifa kila mwaka. Hata ikiongezeka, haitakuwa nyingi sana. Mwisho, kuna watu wanasema kuna nakala tofauti za Mswada huu wa BBI. Hamna. Kosa lilikuwa kwa nambari moja ambayo hata haiko kwenye Katiba. Kwa hayo, nasema shukran. Naunga Mswada huu mkono na nawaomba Wabunge wenzangu wauunge mkono na Wakenya kwa jumla wauunge mkono ukifika kwenye kura ya maoni. Asanteni."
}