GET /api/v0.1/hansard/entries/1065878/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1065878,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1065878/?format=api",
    "text_counter": 98,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Hoja ya nidhamu, Bw. Spika. Taratibu za Bunge la Seneti zinaeleza kwamba huwezi kumtaja yeyote ambaye hayuko ndani ya Bunge au hajaitwa Bungeni na hawezi kujitetea. Je, ni haki kutusi au kutumia lugha isiyofaa kwa viongozi wa Kenya, hususan Baba, Raila Odinga, na kiongozi wa Taifa la Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta? Ni haki kwa kijana ninayemjua na kumpenda sana, ndugu yangu, Sen. Cherargei, Seneta shupavu sana wa Kaunti ya Nandi, kutumia lugha kama hiyo anapojadili ugeuzi huu wa Katiba? Je, kitendo kama hicho ni sawa?"
}