GET /api/v0.1/hansard/entries/1066099/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066099,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066099/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kwamboka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 9246,
"legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
"slug": "beatrice-kwamboka-makori"
},
"content": "Asante Bi Naibu Spika, kwa kunipa fursa hii kuchangia huu Mswada wa marekebisho ya Katiba, 2020. Naunga mkono Mswada huu. Ningependa kuwakumbusha wananchi mahali tumetoka na kwa nini Mswada huu uliwekwa ili tuweze kuujadili. Tukikumbuka wakati tunapo enda katika uchaguzi, baada ya miaka mitano sisi huwa tunapoteza watoto wetu na akina mama wanaaga dunia kwa sababu ya vita. Shida ni kuwa kuna upungufu fulani katika huu Mswada na katika Katiba ya nchi yetu. Ukiangalia Kifungu cha 23 wameweka ubunifu wa nyadhifa za juu. Katika hicho kipengele kuna viti ambavyo vinatakikana viongezwe kama kiti cha Waziri Mkuu na Naibu Waziri Wakuu wawili. Tukiangalia wakati wa uchaguzi huwa tunachagua Rais na mdogo wake. Ikifika wakati wa ugavi wa mali ya hii nchi, mali huwa inaenda katika eneo mbili. Huu Mswada umeletwa kwa madhumuni ya kuleta ujumuishaji. Katika huo ujumuishaji, hizi viti nne zitaenda kwa eneo mbali mbali. Bi Naibu Spika, mwaka 2017, wakati tulipofanya uchaguzi, sisi katika chama chetu cha ODM--- Hata leo nimevaa hii nguo kuonyesha vile tulivyoteseka. Tulikuwa tukitimuliwa na vitoa machozi. Huu Mswada ni mwema sana ---"
}