GET /api/v0.1/hansard/entries/1066101/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066101,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066101/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Bi Naibu Spika nimeskiza kwa makini kabisa, nikamsikia mwenzangu akisema kwamba haya marekebisho kwa Mswada huu yataleta mawiano na hakutakuwa na utengamano. Jambo ambalo anazingatia ni kusema ya kwamba kutakapokuwa na ugavi wa mali katika nchi hii ya Kenya, mali itaenda kwa sehemu nne kulingana na vile ametuambia. Amesema ya kwamba katika Katiba kuna Rais na makamu wake. Kwa hivyo, mali inaenda katika sehemu mbili. Akasema ya kwamba kukiongezwa Waziri Mkuu na manaibu wake, mali itaenda katika sehemu nne. Hii inamaanisha Kenya ina sehemu nne ama wale wananchi wengine wa Kenya hawana manufaa kabisa katika nchi hii?"
}