GET /api/v0.1/hansard/entries/1066108/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066108,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066108/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kwamboka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 9246,
        "legal_name": "Beatrice Kwamboka Makori",
        "slug": "beatrice-kwamboka-makori"
    },
    "content": "Asante Bi Naibu Spika na Seneta wenzangu kwa kumrekebisha mwenzangu hapa ambaye alikuwa anajaribu kuingilia masaa zangu ambayo ninafaa kuchangia. Tukiangalia vizuri, katika Mswada huu kuna viti 70 za eneo bunge ambazo zita ongezwea. Ninaunga mkono kabisa kwa sababu katika jimbo la Nairobi tutaongezewa eneo bunge 12. Ukiangalia idadi ya watu ambao wako Nairobi ni wengi lakini hawajawakilishwa vilivyo kwa sababu zile pesa ambazo wanapata hazitoshi. Ninajua vizuri kwamba tukipata hizo pesa, huu Mswada ukipitishwa nina uhakika bara bara zetu za Nairobi zitakuwa nzuri, watoto wataenda shule, akina mama watapata maji na kutakuwa na maendeleo. Tukiangalia katika huu Mswada pia kuna pesa rasmi ambazo zitakazoenda katika bunge za kaunti. Mimi nilikuwa mbunge wa wadi ya Mountain View mwaka wa 2013 mpaka 2017. Kuna change moto mingi sana katika hizi wodi. Najua wakiongezwa hizo pesa, watoto watasoma, wataweza kujumuika na wananchi waamue vile hizo pesa zitatumika katika kila wodi na wananchi watanufaika. Tukiangalia upande wa Bunge la Seneti ninaunga mkono asilimia mia moja huu Mswada kwa kutuongez akina mama ili tuwe 50-50. Tumechoka kuitwa “flower girls” kwa lugha ya kiingereza. Ikifika wakati wa kupiga kura inapatikana kwamba wale wenzetu ndio wanapiga kura na sisi tunaangalia. Tumechoka, ni wakati wetu akina mama tutoke tupiganie hivi viti kama wanaume kwa sababu tunaweza. Wale wanaopinga, wanaogopa wanawake kwa sababu tuta---"
}