GET /api/v0.1/hansard/entries/1066135/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066135,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066135/?format=api",
"text_counter": 101,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Watu waliweka vidole vyao Kenya nzima katika fomu ambazo zilikuja na kuthibitishe ya kwamba wanaunga mkona Mswada huu. Katika ulimwengu mzima, hakuna Katiba iliyo sawa. Nina maanisha ya kwamba sisi kama wakoloni wa Uingereza, wako na Katiba Nzuri. Lakini sio hao pekee, Waamerika wako na Katiba pia. Lakini, Waingereza waliotutawala hawana Katiba. Wao wanaiita kwa Kizungu un-writtenConstitution . Katiba ya USA ambayo imekuwa ikiwaongoza kwa miaka mingi, mara kwa mara imeweza kufanyiwa--- Jambo la kushangaza ni kwamba ile un-written Constitution ya Uingereza inawaezesha kujitawala. Katika Mswada huu, kuna kasoro kidogo ambayo imeweza kutendeka. Ndio sababu watu wengi wamesema kuigeuza italeta nafuu. Ningependa kukosoa pahali pamoja ambapo panasema mamlaka ya Judicial Service Commission (JSC), ikiongozwa na Jaji Mkuu itakuwa na mamlaka yakuangalia uendeshaji wa ratiba za koti. Mamlaka hayo yamwekwenda kwa Ombudsman . Ni hatari kuona ya kwamba Ombudsman atakuwa na mamlaka ya kumchunguza na hatimaye kumondoa jaji atakayepatika au kuonekana na hatia. Ukweli wa mambo ni kwamba, Ombudsman atakuwa ni chaguo la Rais. Hili ni jambo ambalo watu wanaweza kukaa na kuongea. Katiba ilivyo sasa, kazi ya"
}