GET /api/v0.1/hansard/entries/1066137/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066137,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066137/?format=api",
"text_counter": 103,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "ni ingine. Kwa hivyo, akuwe ndani ya ofisi ya Jaji Mkuu na JSC iachiwe uchapakazi wakutafuta, kuangalia au wakiona kama mwenzao ako na shida ama amepatikana na hatia waandika kwa Rais ili ateua jopo lake analolifikiria kama Tribunal ya kumwangalia jaji na hatimaye chochote kitachotoka hapo kipelekwe kwa Rais na hatua ichukuliwe. Lakini, kwa hivi sasa, hatuoni umaarufu au haraka ya kugeuza sheria kama hiyo. Naibu Spika, kuna mambo mazuri ndani Mswada huu. Jambo la kwanza, kunayo faida ya kuona ya kwamba ugatuzi ndani ya serikali za mashinani umekithiri. Kwa sababu hiyo, kuna bahati ambayo imetoka. Kuna wengine wameweza kupata na wengine wamekosa. Vilevile, jambo kama hili watu wanaweze kuketi chini na kuelewana na kujua ya kwamba kuna wakati mwingine. Watu hawawezi kupata kila kitu ambacho wamekitarajia. Bi Naibu Spika, umuhimu wa hii Katiba ambayo tunataka kuipitisha hivi sasa ni kwamba ina mafanikio mengi. Dada zetu wanaweza kushindana na wanaume wenzao mashinani. Kwa mfano, Naibu Spika, unaweza ‘kuchapana’ na wanaume na kushinda kiti. Lakini namba yenu inakuwa ndogo. Ndio sababu tuliona ya kwamba ni vizuri ndani ya Bunge kuwe na akina mama ambao watachaguliwa na wananchi ambao watakuwa Maseneta. Watakuwa wameteuliwa na wataweza kupiga kura. Hiyo inamaanisha ya kwamba watakuwa 47 wanaume na wanaume. Itaongeza nguvu ndani ya Bunge la Seneti. Hivi sasa kumetokea jinsia ambazo hatuzielewi. Tumeona katika magazeti ya kwamba wanamlaumu Kiongozi wa Waliowachache kwa kupinga BBI. Lakini katika matamshi yake yeye kama wakili, na hapa ndani tukiwa na mawakili waliobobea, ni haki ya wakili kusema kipengele ambacho hakipendezi ili kuwe na marekebisho ili kuwafaa wananchi."
}