GET /api/v0.1/hansard/entries/1066177/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066177,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066177/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wario",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13224,
        "legal_name": "Golich Juma Wario",
        "slug": "golich-juma-wario"
    },
    "content": "Asante Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii niweze kuchangia Mswada ulio mbele yetu. Kwanza, ningependa kuwapa pole waliokufa kwa sababu ya ugonjwa wa Corona. Ninawafariji na kuwatakia uponaji wa haraka walio hospitalini ili waweze kujumuika na jamii zao. Ningependa pia kuwapa heri njema Waislamu wote katika Kaunti ya Tana River, nchi ya Kenya na dunia kwa jumla. Saum maqbul, waramadan karim. Ningependa pia kumtakia janatul firdaus mwenyekiti wa BBI, Sen. Haji, kwa kunakili Ripoti hii. Yuko mbele ya Mwenyezi Mungu, ninaomba ampe pepo huko aliko mbele ya haki. Kuna mambo mazuri ndani ya Ripoti ya BBi lakini kunayo mengi ambayo yanahitaji kuboreshwa, kupigwa msasa na kubadilishwa ili Ripoti hii iwe nzuri. Bila kupiga msasa, Ripoti iliyo mbele yetu itatufinya sisi wengine na kutuweka katika hali ya utatanishi katika sehemu tunayowakilisha. Sehemu ninayowakilisha ya Tana River imewachwa nyuma kimaendeleo kwa miaka mingi. Sehemu yake ni kubwa lakini kulingana na idadi tuko wachache. Kama ripoti aitawasaidia wale wachache walioko katika kaunti kubwa, mimi nikifika Tana River nitajipata katika hali mbaya ya kujichoma kwa maji ya moto. Nikiiunga mkono katika Seneti hii, nitajitia kitanzi kwa sababu Mswada uliopita ya ‘mtu mmoja, shilingi moja’ inakaba koo watu wa Tana River na watapoteza ugavi wa pesa. Ndio moja ya zile losing counties . Kwa hivyo, nikiwa mwakilishi wa losing county na niunge mkono, basi nikienda nyumbani nitatiwa kitanzi. Mambo haya yanajiandika na sio mzaha. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}