GET /api/v0.1/hansard/entries/1066182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066182/?format=api",
"text_counter": 148,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "Asante rafiki yangu mpendwa, Sen. Kinyua. Kiswahili kinaendelea kukua kila siku. Unavyonisikiza, hapa nilipo hakuna kukuru kakara. Mambo yamepoa kama maji baridi iliyo ndani ya mtungi. Sauti yangu inabobea vizuri. Ndio sababu ninasema hakuna makelele huku na kule. Seneti ikiwa na fedha na ikiboreshwa vizuri, tutaweza kukagua fedha zinazoenda kwa kaunti. Hii ni kwa sababu kutakuwa na National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF) kama ilivyoandikwa kwa Ripoti hii na pia pesa hizi zitaenda hadi kwa wadi. Inatakikana Seneti ifanya uchunguzi na ukaguzi. Kama ofisi ya Seneta haitakuwa na nguvu ya kutembea na kuangalia yale yanafanywa mashinani, Seneti itakuwa na nguvu. Kulingana na mimi, Seneti ambayo itawakilishwa na mama na baba itakuwa na idadi kubwa. Lakini, kuboreshwa kwa uchunguzi kutafanya iwe mwenyekiti mwenza wa mwingine ili ofisi hio iweze kuwakilishwa katika Seneti na mashinani ili iwe na nguvu zaidi na iweze kuzungumza maswala ya kaunti katika Seneti jijini Nairobi. Ndio sababu nilisema Mswada huu unahitaji koboreshwa na kupigwa msasa ili ukae vizuri zaidi. Bi Spika wa Muda, nina wakilisha Kaunti iliyoachwa nyuma kimaendeleo kwa muda mrefu sana. Tangu Kenya ipate uhuru hadi leo, hospitali hazifanyi kazi vizuri katika Kaunti ya Tana River na pia watu wako mbali na huduma. Utalazimika kutembea mwendo mrefu kutafuta hospitali na vile unavyojua, hakuna barabara hasa msimu huu wa mvua. Iwapo pesa za Kaunti zitapunguzwa ama tukose kupata nyongeza kupitia Mswada huu, basi mambo yangu yataenda vibaya. Ndiyo sababu tunasema, tuupige msasa ili tuuboreshe Mswada huu. Bi. Spika wa Muda, kama nyongeza ya maeneo Bunge 70 ilizingatia zaidi idadi ya watu, kusema kweli mimi ninaangukia hapo. Iwapo hesabu zote zitazingatia tuu idadi ya watu na viti vingi vipelekwe katika sehemu zenye watu wengi, basi kuna Wakenya ambao hawata wakilishwa katika Bunge la Taifa kwa sababu ni wachache katika Kaunti kubwa. Mahitaji yao maalum hayatawasilishwa wala kupata nafasi Bungeni. Katika hali hiyo, tutaendelea kuwa nyuma. Katika kupiga msasa na kuboresha idadi ya watu katika Bunge la Kitaifa, nilitaka tuangalie hicho kipengele sana. Tuangalie sehemu zenye mahitaji maalum, kama ukosefu wa mvua. Wakati mwingi, Kaunti ya Tana River hupata tuu maji kutoka kwa mabwawa saba yaliyowekwa katika nyanja za juu za Mto Tana. Mara kwa mara, tunapata mafuriko na watu wanalazimika kuhama na baadaye kurudi manyumbani mwao. Sehemu kama hizo pia ziangaliwe kama zenye mahitaji maalum, tofauti na sehemu zingine. Baada ya hapo, wapewe kiti ili wasikike katika Bunge la Kitaifa ili nasi tuwe na nchi ya kujivunia. Ripoti hii haikusema hivyo bali iliendelea tuu kuongeza viti katika sehemu ambazo tayari zishaendelea tangu Kenya ipate uhuru. Hizi ni sehemu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}