GET /api/v0.1/hansard/entries/1066183/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066183,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066183/?format=api",
"text_counter": 149,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13224,
"legal_name": "Golich Juma Wario",
"slug": "golich-juma-wario"
},
"content": "ambazo ziko na barabara, hospitali, shule na vyuo vikuu vizuri. Huko ndiko haya maeneo mapya ya Bunge yamepelekwa. Sisi hatujapata hata kiti kimoja cha kushughulikia mahitaji maalum kama watu tuliotengwa kwa muda mrefu. Katika kupiga msasa Mswada huu, hivyo ndivyo mimi na watu ambao ninawakilisha tungesaidika. Ingejumuisha pia wale wanaofanana na mimi, kama vile huko North Horr ambapo ni sehemu kubwa na hata kaunti za Marsabit, Isiolo na Wajir. Katika sehemu hizo, utapata wafugaji wengi wa kuhamahama na mahitaji yao ni tofauti na ya Wakenya katika sehemu zingine. Maswala yayo hayo ndiyo pia yangepata nafasi ya kuzungumziwa katika Bunge la Taifa. Iwapo tungefanya hivyo, basi Mswada huu ungetusaidia na tungesherehekea kama Wakenya wengine na kusema tuupigie kura kisha tuendelee. Hilo halikupatikana katika Mswada huu. Bi. Spika wa Muda, hata wewe mwenyewe ukiangalia, sio ati tunazungumza tu hapa lakini pia kuna kusema na kutenda. Kuna mahitaji maalum ambayo hakika, hayakufika katika Ripoti hii. Kwa hivyo, dosari nyingi zinaonekana. Kwa kweli ukiangalia Mswada huu, waliouandika walipoteza wakati wao mwingi. Walikaa usiku na mchana na kuzunguka lakini mahitaji yetu hayajawekwa katika Mswada huu. Ukiangalia hivi, hatuna sababu kamwe ya kusema Mswada huu upite. Ni lazima tuwekewe madaliko hayo. Bi Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi."
}