GET /api/v0.1/hansard/entries/1066256/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066256,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066256/?format=api",
"text_counter": 222,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Naunga kuongeza maeneo bunge mia kwa mia. Hii ni kwa sababu Laikipia, Ruiru, Kieni na Kipipiri zina watu zaidi. Ni vizuri tujue ya kwamba huduma inapewa watu na sio sehemu. Hapo ndipo tulisimama kidete tukisema, ‘ one man, one vote, oneshilling.’ Hii ni kwa sababu afya inapewa mwananchi na mwananchi ndiye atapita katika hiyo barabara. Hii ndio kwa sababu mimi naunga mkono kuongezwa kwa hayo sehemu 70. Eneo bunge ya Laikipia Magharibi iko na watu zaidi ya 100,035 na wanawakilishwa na Mbunge mmoja. Katika sehemu zingine humu nchini, utapata ya kwamba mbunge anawakilisha watu 40,000. Kwa hivyo, lazima tutoshane. Waswahili wanasema mgala muue na haki umpe. Lazima tupewe haki kwa sababu sisi sote ni wakenya na tunapaswa kuwakilishwa kwa sababu tunalipa ushuru kama wenzetu. Tumekuwa tukiambiwa ya kwamba vijana ambao wamemaliza chuo kikuu hawata lipa pesa ambayo walipewa na Higher Education Loans Board . Mimi naonelea ya kwamba serikali ingewasaidia kupata kazi badala ya kuwaambia eti wasilipe hiyo pesa. Ni vizuri wapate ajira ndiposa waweze kulipa hiyo pesa. Mimi ni Seneta wa Laikipia na ninasumbuka rohoni kwa sababu ninaongea kuhusu marekebisho ya Katiba ilhali watu wangu wanaendelea kuvamiwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama. Watu wangu wana uawa. Kuna watu ambao walishambuliwa jana. Kwa hivyo, nasikia ugumu kujadili mambo ya Katiba ilhali watu wamenituma hapa kuongea mambo ya usalama wao. Wanataka niulize vile watapata ajira. Huu ni msimu wa kupanda na watu hawana fertilizer . Sahizi, tungekuwa tunaongea maswala ambayo yanahusu wakenya na sio maswala ambayo yangejadiliwa baada ya hii ugonjwa. Tunasema ya kwamba tutaongeza pesa katika kaunti na hiyo ni nzuri. Tumekuwa tukiangalia pesa ambazo zimetumika katika wakati huu wa Covid-19 na unapata ya kwamba kaunti nyingi hazitumii pesa inavyotakikana. Kwa hivyo, ingekuwa vizuri kama BBI ingependekeza ya kwamba maseneta wapewe tita la hela ya kufanya kitu ambacho kinaitwa oversight . Wabunge wako na pesa za National Government ConstituenciesDevelopment Fund lakini Seneta hana lolote. Kazi yake ni kutembea na kuangalia miradi bila chochote. Ninaunga mkono pesa ambazo zinaenda kwa wajumbe wa wadi, ambayo inaita"
}