GET /api/v0.1/hansard/entries/1066261/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066261,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066261/?format=api",
"text_counter": 227,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Pole sana, Bw. Spika wa muda. Sikumaanisha hivyo. Nilikuwa ninalinganisha. Sikumaanisha ya kwamba huwezi kustahimili chumvi. Marekebisho yaliyoko katika Katiba ambayo tunajadili siku ya leo inasema ya kwamba kaunti haiwezi ikapata mara tatu ya vile ambavyo pesa zimepeanwa. Ni vizuri hii ijulikane na ninaiunga mkono kwa sababu sisi sote tuko sawa katika nchi hii. Sehemu ambayo ninawakilisha imebaki nyuma kwa muda mrefu. Sehemu ambayo mimi nawakilisha imebaki nyuma kwa muda mrefu. Wakati umefika wa sisi kuweza kunufaika kwa sababu sisi wote ni Wakenya na Wakenya wote wana haki ya kuamini kwamba sisi sote ni Wakenya. Ninajua Kaunti ya Kiambu nyinyi mmekuwa na shida nyingi. Unapata mtu mmoja anapata Kshs5,000 na ukiangalia sehemu zingine mtu mmoja anapata zaidi ya Kshs17,000 pesa zikigawanywa. Hiyo sio haki. Kwa hivyo, ni vizuri mambo yote yalinganishwe na sisi zote tuseme ya kwamba sisi ni Wakenya ndio tuweze kutembea pamoja. Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda."
}