GET /api/v0.1/hansard/entries/1066685/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066685,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066685/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, zote ziko wazi kwa wananchi. Lakini, ikiwa tumekaa Bungeni maelezo yale yatakuwa yanapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga hadi Wajir ambako watu hawataweza kuja hadi Nairobi kusikiza kesi ambayo iko dhidi ya gavana wao. Justice must not only be done, but seen to be done . Kwa hivyo, haki itatendeka wakati Bunge lote la Seneti litakapo kaa kuchunguza madai ambayo yameletwe mbele ya Bunge hili kuhusiana na gavana yeyote yule. Kanuni zetu zinafaa zibadilishwe. Gavana akipatikana na hatia, anatakikana aje kujitetea lakini madai yasipothibitishwa, Bunge halitapata fursa ya kujadili ripoti ile. Kwa hivyo, Bunge itakuwa kama conveyor belt . Tutasomewa mashtaka, alafu iende kwa Kamati na baada ya hapo, hatuna jukumu lolote isipokuwa kunyamaza. Hii ni kinyume na kukaa hapa kama Maseneta wote wa Jamhuri ya Kenya kuchunguza na kuhakikisha haki inatendeka. Mimi naunga mkono Bunge nzima la Seneti kuchunguza swala hili la Wajir."
}