GET /api/v0.1/hansard/entries/1066823/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066823,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066823/?format=api",
    "text_counter": 36,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Waheshimiwa Maspika, ninamshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutujalia afya na uhai na kutupatia kibali kilichotuwezesha kukutana hapa siku ya leo. Niko na furaha kubwa leo kupata nafasi ya kuhutubia Kikao cha Pamoja cha Bunge la Taifa na Bunge la Seneti la Jamhuri ya Kenya. Kabla sijaendelea, niruhusu nitangulize shukrani zangu kwako, Mhe. Kenneth Lusaka, Spika wa Bunge la Seneti, na, Mhe. Justin Muturi, Spika wa Bunge la Taifa, kwa kuitisha Kikao hiki cha Pamoja cha Bunge na kunialika mimi kuhutubia. Kupitia kwenu, ninawashukuru Waheshimiwa wabunge la Taifa na Bunge la Seneti, kwa kuridhia kwa kauli moja kufanyika kwa Kikao hiki. Asanteni sana!"
}