GET /api/v0.1/hansard/entries/1066827/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066827,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066827/?format=api",
"text_counter": 40,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Ninatambua kwamba huu sio utaratibu wa kawaida wa Kenya. Sio kila Rais anayefanya ziara rasmi hupewa heshima hii ya kuhutubia Bunge, tena Kikao cha Pamoja cha mabunge yenu mawili. Wenzetu mna Bunge lenye Chambers mbili, sisi wenzenu tuko na Bunge moja tu. Kwangu, itakuwa ndio mara ya kwanza kuhutubia Chambers mbili za Bunge kwa pamoja. Sio jambo ndogo na ni heshima kubwa iliyoje. Mmenipa heshima kubwa sana. Nimefarijika kuwa nimepata nafasi hii mwanzoni mwa uongozi wangu. Niseme kuwa kumbukumbu hii haitafutika kwenye maisha yangu. Asanteni sana!"
}