GET /api/v0.1/hansard/entries/1066829/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066829,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066829/?format=api",
    "text_counter": 42,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Uamuzi wenu wa kunipa fursa hii ni kielelezo cha thamani na uzito ambao mnaupa uhusiano mzuri uliopo kati ya nchi zetu mbili. Niwahakikishieni kuwa nasi tumeguzwa sana na heshima, upendo na ukarimu mkubwa ambao mmetuonyesha. Wema huacha deni na deni lake ni kulipwa kwa wema. Sisi Tanzania, tutalipa wema huu. Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge, sitatenda haki nisipomshukuru kipekee ndugu yangu, Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta. Rais Kenyatta ni miongoni mwa viongozi wa mwanzo kabisa walionipigia simu kunifariji mara tu baada ya kusikia taarifa ya kifo cha aliyekuwa Rais wetu mpendwa, Hayati Mhe. (Dr.) Magufuli. Kama haikutosha, hakusita kukatiza ratiba yake na kufika yeye binafsi kushiriki nasi katika msiba wa kitaifa kule Dodoma. Siku ile, alitufariji sana kwa maneno yake na salamu zake za buriani kutoka kwa wananchi wa Kenya. Hatutasahau pia kitendo chake cha kutukumbusha umuhimu wa kuheshimu dini na imani za wengine."
}