GET /api/v0.1/hansard/entries/1066831/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066831,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066831/?format=api",
    "text_counter": 44,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Uhuru Kenyatta alisitisha kuhutubia akiwa jukwaani, ili kupisha adhan iliyokuwa ikisomwa Msikitini imalizike na ndio akaendelea. Alituwachia gumzo na funzo kubwa sana kwetu. Alitumia jukwaa lile kunipongeza kwa kushika dhamana hii ya Urais ya Awamu ya Sita ya Tanzania. Aliahidi kunialika nchini Kenya mara baada ya kipindi cha maombolezo kumalizika. Rais Kenyatta ni mtu wa kutimiza ahadi. Mara tu baada ya kumalizika kipindi cha maombolezo, alinitumia ujumbe maalum kuniona, ambao pia uliambatana na mwaliko wa kutembelea Kenya. Na mimi nimekuja Kenya kuitika wito wake. Mimi na ujumbe wangu tumepata mapokezi mazuri sana toka tulipowasili Jijini Nairobi. Tumejisikia tuko nyumbani haswa. Tumepokewa kwa ukarimu mkubwa na hio ndio hulka, desturi na asili ya watu wa Kenya. Nimebaini kuwa sehemu kubwa ya ujumbe nilioambatana nao, wanajua vichochoro vya Jiji la Nairobi. Wanajua nyama choma inapatikana wapi. Lakini kutokana na Korona, hawakuweza kujibamba. Nina wasiwasi nisije nikawabakisha nyuma."
}