GET /api/v0.1/hansard/entries/1066834/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066834,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066834/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Tunawashukuru kwa yote; mapokezi na ukarimu mkubwa. Jana nilifanya kikao na Mheshimiwa Rais Uhuru Kenyatta na ujumbe wake wa viongozi wa Serikali. Tumekuwa na mazungumzo mazuri yenye kuamsha matumaini makubwa kwa mashirikiano kati ya nchi zetu mbili kwa siku zijazo mbele yetu. Hapakuwa na ugumu wala ukakasi wowote katika kufikia mwafaka wa mambo tuliyokuwa tukijadiliana. Tumezungumza kwa kindugu sana. Kilichojitokeza wazi katika mazungumzo yale ni namna ambavyo nchi zetu mbili zinakubaliana katika mambo mengi kuliko yale machache sana tunayotofautiana. Hata hayo machache tunayotofautiana, yenyewe hayakuwa na misingi imara ya tofauti ila ni mitazamo tu ya watu. Mitazamo nyingi ambayo inaleta ukakasi huchangiwa kutokana na kukatika kwa mawasiliano baina ya nchi zetu mbili. Sasa ili kuondoa mikakati hasi kati yetu, tumekubaliana kujenga na kuendeleza utamaduni wa kukutana mara kwa mara katika ngazi zetu mbali mbali. Ndugu na jirani wanaotembeleana hujenga ukaribu kuliko wale wasiotembeleana. Umbali hujenga mashaka na ukaribu huondosha mashaka hayo. Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge, kama nilivyosema, hii ni ziara yangu ya kwanza rasmi nchini Kenya tangu kushika wadhifa wa uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 19.03.2021. Ipendeze kusema kuwa itaingia katika kumbukumbu za kihistoria kuwa Kenya ndio nchi ya kwanza kwa raisi wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya ziara rasmi. Nilikwenda Uganda kwa mathumuni maalumu ya kusaini mktaba."
}