GET /api/v0.1/hansard/entries/1066842/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066842,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066842/?format=api",
"text_counter": 55,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Lakini zaidi, kuna Mohamed Faki Mwinyihaji ambaye ni Seneta wa Mombasa na jina lake ni jina safi la Kizanzibari. Kwa hivyo, hatuwezi kutengana. Hiyo ni mifano chache tu. Fundo la pili ni historia. Kabla ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, 1967, nchi zetu mbili hizi tayari zilisha kuwa chini ya East Africa Common ServiceOrganization (EACSO) zikiwa chini ya utawala wa Kikoloni wa waingereza. Huduma zetu muhimu, miundo mbinu yetu na uchumi zetu, zilifuma pamoja kabla hata nchi zetu hazijapata uhuru. Fundo la tatu ni jiogrofia. Mwenyezi Mungu amejalia nchi zetu mbili hizi kuwa majirani. Tuna mipaka ya baharini na mipaka ya ardhini. Na hata ekolojia yetu ni moja. Ndio kusema kuwa hata wanyama pori wetu ni ndugu na ni majirani. Kuna wale wanyama pori ambao huja kupata mimba Kenya na wanarudi kuzaa Tanzania."
}