GET /api/v0.1/hansard/entries/1066845/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066845,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066845/?format=api",
    "text_counter": 58,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Kutokana na ukweli huo, ushirikiano wetu sio wa hiari bali ni wa lazima kutokana na kanuni ya uasili wa undugu ambao Mwenyezi Mungu ameumba. Ushirika na ujirani yote yanatufanya tuwe pamoja. Hali ya maumbile, hatuna uwezo wa kubadilisha. Iliyobaki ni tupendane au tuchukiane, tuzungumze au tununiane, hatuwezi kukwepa kutokana na mafundo hayo matatu tuliyowekwa nayo pamoja."
}