GET /api/v0.1/hansard/entries/1066846/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066846,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066846/?format=api",
    "text_counter": 59,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Tunategemeana kwa kila hali. Iwe heri au iwe shari. Iwe neema au dhiki, tunategemeana. Panapotokea ukame Tanzania, njaa inabisha hodi Kenya. Uzalishaji wa viwanda ukisimama Kenya, bidhaa zinakosekana Tanzania. Kwa hivyo, tunategemeana. Hivyo, hapana budi ila tupatane na tuelewane ili tuishi kwa pamoja kwa neema na furaha. Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge, binafsi huwa nashangazwa sana na wale ambao wanadhani eti Kenya na Tanzania ni washindani, kwa hivyo, uhusiano wetu unapaswa kuwa wakuhasimiana na kukamiana."
}