GET /api/v0.1/hansard/entries/1066850/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066850,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066850/?format=api",
    "text_counter": 63,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Tunawaalika kwa sababu Tanzania ina mambo mengi; ina rasilmali za kutosha, madini ya kutosha, ardhi kubwa na mambo mengi mengine,tunakosa mtaji. Kenya mna mtaji wa kutosha. Karibuni Tanzania. Dhamira yangu ya kuja nchini Kenya ni kuzungumza na nyinyi na kuona namna gani Watanzania wataweza kufanya vizuri zaidi nchini Kenya. Mbali na uwekezaji, ushirikiano wetu kwenye sekta ya biashara nao ni mkubwa na umeendelea kushamiri siku hadi siku. Usafirishaji wa bidhaa za Tanzania kwenda Kenya umeongezeka kutoka Tshs309.6 billioni mwaka 2017 hadi Tshs526.3 billioni mwaka 2020. Kwa upande wa Kenya nayo iliongeza kiwango cha kuuza bidhaa zake nchini Tanzania kutoka Tshs420 billioni mwaka 2007 hadi Tshs571 billion mwaka 2020. Hii inatusuta sisi viongozi na wanasiasa. Inatuonyesha kuwa wananchi wa nchi zetu mbili daima wako hatua mbele yetu. Wanafanya biashara zao kwa ubunifu mkubwa lakini sisi tunang’ang’ana na sheria na vikwazo na mambo kama hayo na tunawavuta"
}