GET /api/v0.1/hansard/entries/1066852/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066852,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066852/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "nyuma kidogo. Ni wakati sasa wa sisi viongozi kubadilika tuwe daraja la kuunganisha watu wetu na sio tuwe vikwazo kwao. Mimi na ndugu yangu Rais Uhuru Kenyatta tumekubaliana kuweka utaratibu madhubuti wa kuzuia na kukabiliana na zile pilka pilka pale zinazotokea katika mipaka yetu wakati wa kuvusha biashara kwenda na kurudi katika nchi zetu mbili. Waheshimiwa Spika, Maseneta na Wabunge mashirikiano ya uwekezaji na biashara ni sehemu tu ya mashirikiano mazuri kati ya nchi zetu. Utalii ni eneo nyingine ambayo tunapaswa kushirikiana sana. Kama nilivyogusia ekologia zetu zinaingiliana. Hivyo hivyo, ukaribu wa vivutio vyetu vya utalii na vyenyewe vinaingiliana. Tunayo nafasi ya kunemeka pamoja ikiwa tutashirikiana katika sekta hii kuliko kushindana. Badala ya kunyang’anyana idadi ya watalii busara inatutaka tuelekeze nguvu zetu kuhamasisha mtalii aongeze idadi ya siku ambazo atazitumia nchini Kenya na Tanzania. Kwa kufanya hivyo, sote tutafaidika. Kama alivyowahi kusema Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alisema na ninanukuu: “Tukipoteza muda mwingi kugawana kibaba - kibaba ni kipimo cha kupimia kama mchele, ngano, sembe.” Anasema tukipoteza muda mwingi kugawana hicho tutapoteza muda mzuri sana wa kuvuna kipimo kikubwa zaidi. Mashirikiano yetu yanashamirishwa pia na jitihada kubwa tunazochukua katika vita dhidi ya uhalifu, ujangili, ugaidi, madawa ya kulevya na uharamia Bahari ya Hindi na katika Ziwa la Victoria. Kwa vile muhalifu wa Kenya na Tanzania wana mashirikiano mazuri basi hakuna budi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama navyo vishikamane na wawe na mashirikiano mazuri ili tuweze kulinda maeneo yetu na kushinda ushirikiano wa wahalifu. Mashirikiano haya mazuri baina ya vyombo vyetu yamechangia sana kuwepo kwa utulivu na kutoa fursa kwa shule za kibiashara na uwekezaji kushamiri. Kenya ikiwa salama na sisi Tanzania tuko salama. Hali kadhalika, Tanzania ikiwa salama, Kenya nayo inakuwa salama. Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge, ujenzi wa miundo mbinu ya pamoja ni sehemu ya jitihada zetu za kuimarisha mashirikiano yetu ya kiuchumi na kimikakati. Miradi hii inajumuisha kwa uchache miradi ifuatayo: Kwanza ni ujenzi wa barabara ya lami kutoka Lamu-Mombasa kupitia Tanga-Bagamoyo hadi Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 454 chini ya programme ya Jumuiya ya Africa Mashariki ya kuendeleza miundo mbinu ya bara bara kwa nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki. Katika ushorodha wa pwani - yaani coastal corridor - kwa upande wetu tuko mbioni kukamilisha ujenzi wa kipande cha Pangani-Bagamoyo na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 124.5. Tayari tumekwisha pata fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jana nilikuwa na mazungumzo na kaka yangu Uhuru naye anamalizia mazungumzo ya kupata fedha ili kazi hii ianze kwa upande wa Kenya na tukutane pale kwenye mpaka. Mradi wa pili ni barabara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi, yenye urefu wa kilomita 260. Mradi huu ni sehemu ya mradi wa maendeleo ya barabara ya Arusha-Namanga-Athi"
}