GET /api/v0.1/hansard/entries/1066854/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066854,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066854/?format=api",
"text_counter": 67,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "River iliyofunguliwa rasmi mwaka wa 2002. Mradi huu unatekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza imeshakamilika, sasa tunajipanga kuendelea na awamu ya pili ya mradi huu. Mradi wa tatu, tunavyo vituo vya huduma vya pamoja mpakani vya Namanga: Namanga West BP na Holili Taveta West BP. Vituo hivi vimerahisisha shughuli za biashara mipakani na uvukaji wa watu. Nafurahi kuona vituo hivi vimekuwa chachu ya shughuli za kiuchumi katika maeneo ya mipaka ya mipaka yetu. Tunaendela na mchakato wa kukamilisha mifumo ya vituo vya Horohoro, Lunga Lunga na Sirari-Isebania ili navyo viweze kutoa huduma kwa wepesi na kwa ufanisi. Mradi wa nne ni wa kusafirisha umeme mkubwa wa Kw400. Kwa upande wa Tanzania mradi unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme kutoka Singida hadi Namanga. Ujenzi wa kituo kipya cha kuposia umeme mjini Arusha na eneo la Legumor na upanuzi wa kituo cha kuposia umeme cha Singida. Kwa upande wa Kenya, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya umeme msongo wa KW400 inayojengwa kutoka kituo cha kupozia umeme cha Isinya hadi Namanga yenye urefu wa kilomita 94, inayounganishwa na njia ya umeme inayojengwa upande wa Tanzania. Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan, zimekubali kugharamia miradi hiyo. Mradi mwigine – Mwenyezi Mungu akijalia Inshallah - Serikali zetu mbili zitaanza kutekeleza mradi wa bomba la gesi, kuitoa gesi Dar es Salaam hadi Mombasa. Mazungumzo ya kutafuta fedha kwa ajili ya mradi huo yanaendelea. Tunatarajia yatakamilika mapema inavyowezekana."
}