GET /api/v0.1/hansard/entries/1066884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066884,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066884/?format=api",
"text_counter": 97,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "kutoelewana kati yetu, tunadhohofisha Jumuia ya Afrika Mashariki. Bila kukusudia, tunajikuta pia tunaathiri kasi ya utangamano wa Afrika Mashariki; hivyo hatuna budi kuendelea kuelewana. Nikiri kwamba kuna nyakati ambapo ushirikiano wa Afrika Mashariki ulijaribiwa, ambapo baadhi ya matukio, kauli na vitendo vyetu, viliweka majaribuni mahusiano yetu na kuupima uimara wa dhamira zetu za kuendelea na safari yetu ya utangamano. Ninachofarijika ni kwamba katika nyakati zote hizo, kwa busara za viongozi waliotutangulia, na kwa imara wa mafundi wa uhusiano wetu, tulishinda na dhamira yetu iliimarika zaidi. Uchungu wowote uliojitokeza pale ambapo tulijaribiwa, ulikuwa ni uchungu wa uzazi na sio uchungu wa maradhi. Kwa maana kwamba, uchungu wa uzazi unaishia kupata mtoto na kuleta furaha kwenye familia. Lakini uchungu wa maradhi unaishia kwenye kifo. Kwa hivyo sisi tunapokerana, uwe uchungu wa uzazi. Tukae, tuzungumze na tupate mtoto, amani, na tuendelee na uhusiano wetu."
}