GET /api/v0.1/hansard/entries/1066886/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066886,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066886/?format=api",
    "text_counter": 99,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Niwahakikishie kuwa mimi na wenzangu nchini Tanzania tutafanya kila linalowezekana ili uhusiano wetu uzidi kungaa’ na kwa kufanya hivyo, tung’arishe ushirikiano wa Afrika Mashariki. Tanzania itaendelea kuwa jirani, pia na rafiki muaminifu wa Kenya na mwanachana muadilifu na wakutumainiwa ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Jitihada zangu na wenzangu katika serikali ninayoiongoza zitaelekezwa katika kuimarisha ushirikiano wetu ndani ya Jumuia yetu ya Afrika Mashariki. Tutaelekeza jitihada zetu katika kutafuta majawabu palipo na changamoto, kufufua fursa palipo na vikwazo na kuleta matumaini palipo na mashaka. Tutafanya hivyo kwa kuamini kwa dhati kabisa kuwa wana Afrika Mashariki hatima yetu imefungamana nasi hatuna budi tufungamane. Ombi langu kwenu waheshimiwa wabunge kama nilivyosema awali, mtusaidie kutimiza adhima hiyo. Sisi tulioko serikalini, mtusukume tutekeleze wajibu wetu huu wadhimu na pale tunapo zubaa, msisite kutukosoa. Nanyi pia tunawaomba mtimize waajibu wenu. Mtusaidie kutunga sheria na kushawishi serikali zetu kuhusu sera zinazochochea na kuwezesha mtangamano. Tusiruhusu na tukemee misimamo, mitazamo na kauli za baadhi ya wanasiasa ndani ya mabunge yetu ya kuleta mgawanyiko na kudhohofisha Jumuia ya Afrika Masharika."
}