GET /api/v0.1/hansard/entries/1066893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066893,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066893/?format=api",
"text_counter": 106,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Nitakuja kusema maneno mengine mbele tukikutana. Kwa hivyo siishi hapa bali nahairisha maneno yangu hapa. Tunapokutana Watanzania na Wakenya, kuna mambo mengi; utani unakuwa humo na vijembe viko humo. Hayo ndiyo mambo yanayochangamsha uhusiano wetu. Sina shaka kuwa tutapata fursa ya kuyazungumza mengi zaidi na kwa kina katika majukua mengine tutakayokutana. Natumia fursa hii kwa mara nyingine tena kuwashukuru waheshimiwa maspika kwa mara nyingine tena kwa kunikaribisha. Lakini namshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa mwaliko wa kuniomba mimi kufanya ziara hii rasmi ya kiserekali nchini Kenya. Nataka niwadhibitishie kwamba tumevuna mengi na makubwa sana katika ziara hii. Ziara hii imefungua milango mingi sana. Lililobaki, mtusimamie kwenye utekelezaji. Nami nimemualika Rais Uhuru Kenyatta aje Tanzania mwezi wa Desemba mwaka huu. Tanzania itatimiza miaka 60 ya uhuru mwaka huu. Nimemualika Rais Uhuru Kenyatta aje kwenye sherehe hizo kama mgeni wetu maalum. Kama nilivyosema, natumia fursa hii kuwashukuru maspika; Mhe. Kenneth Lusaka na Mhe. Justin Muturi kwa makaribisho yenu mazuri sana ndani ya bunge. Nawashukuru pia Maseneta na wabunge wa Bunge la Taifa kwa kutenga muda wenu adhimu kunikaribisha kuzungumza nanyi. Kupitia kwenu, nawashukuru ndugu zetu, wananchi wa Kenya kwa mapokezi mazuri waliotupatia. Tunaondoka Kenya na kumbukumbu nzuri ya ziara hii na shauku kubwa ya kurudi tena siku zijazo. Hii ni ziara yangu ya kwanza nchini Kenya, nawaahidi kuwa haitakuwa ya mwisho. Kwa maana hiyo, nasema, udumu undugu wa Kenya na Tanzania na wadumu viongozi wetu. Mungu aibariki Jamhuri ya Kenya. Mungu aibariki. Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Asanteni sana kwa kunisikiliza."
}