GET /api/v0.1/hansard/entries/1066946/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066946,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066946/?format=api",
    "text_counter": 42,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "mikakati hasi kati yetu, tumekubaliana kujenga na kuendeleza utamaduni wa kukutana mara kwa mara katika ngazi zetu mbali mbali. Ndugu na jirani wanaotembeleana hujenga ukaribu kuliko wale wasiotembeleana. Umbali hujenga mashaka na ukaribu huondosha mashaka hayo. Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge, kama nilivyosema, hii ni ziara yangu ya kwanza rasmi nchini Kenya tangu kushika wadhifa wa uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 19.03.2021. Ipendeze kusema kuwa itaingia katika kumbukumbu za kihistoria kuwa Kenya ndio nchi ya kwanza kwa raisi wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya ziara rasmi. Nilikwenda Uganda kwa mathumuni maalumu ya kusaini mktaba."
}