GET /api/v0.1/hansard/entries/1066948/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066948,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066948/?format=api",
"text_counter": 44,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Haikuwa ziara rasmi. Ziara yangu rasmi ya kwanza nimeanza na Kenya. Kwa lugha nyingine, mguu wangu wa kwanza kutoka nje kwa ziara rasmi umeanza Kenya. Jana nilikaribiswa Iftar na Mheshimiwa Rais na baadaye tukawa na chakula cha usiku. Dua nyingi zilisomwa na baada ya kumaliza kusoma dua, mvua ilinyesha. Ilikuwa baraka sana. Mungu ameweka baraka kwenya ziara yangu na yale yote ambayo tumezungumza. Kwa hivyo, tumshukuru Mungu. Uamuzi wangu wa kuja Kenya, kuwa nchi ya kwanza, sio wa bahati mbaya wala ni wa makusudi. Busara inaelekeza kuwa ukiwa mpangaji mpya kwenye eneo, lazima ujitambulishe kwa majirani."
}