GET /api/v0.1/hansard/entries/1066951/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066951,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066951/?format=api",
"text_counter": 47,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Uhusiano wa Tanzania na Kenya ni wa kipekee sana. Ni uhusiano uliofungwa katika mafundo matatu. Fundo la kwanza ni undugu wa damu kati ya wananchi wetu wa pande mbili ambao hauwezi kutenganishwa na mipaka ya kuchorwa kwenye ramani. Makabila ya pande mbili za mpaka yanaingiliana na watu wake ni wale wale wamoja. Tanzania inapakana na nchi nane, lakini ni nchi ya Kenya pekee ndio ambayo tunajamii nyingi zilizopo katika pande mbili za nchi zetu. Kwenye Ukumbi huu wa Bunge, nadhani ndani hapa kuna akina Otieno, Boke, Namelok kama ilivyo Tanzania. Lakini pia kuna akina Kilonzo na Kioko kama ilivyo Tanzania."
}