GET /api/v0.1/hansard/entries/1066959/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066959,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066959/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Tunategemeana kwa kila hali. Iwe heri au iwe shari. Iwe neema au dhiki, tunategemeana. Panapotokea ukame Tanzania, njaa inabisha hodi Kenya. Uzalishaji wa viwanda ukisimama Kenya, bidhaa zinakosekana Tanzania. Kwa hivyo, tunategemeana. Hivyo, hapana budi ila tupatane na tuelewane ili tuishi kwa pamoja kwa neema na furaha. Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge, binafsi huwa nashangazwa sana na wale ambao wanadhani eti Kenya na Tanzania ni washindani, kwa hivyo, uhusiano wetu unapaswa kuwa wakuhasimiana na kukamiana. Nawashangaa wanaodhani kuwa Kenya pekee yake ama Tanzania pekee yake inaweza endelea bila mwenzake. Mbaya zaidi ni kule kuamini kwao ya kwamba hiyo inawezekana tu mmoja wetu kumuangusha mwenzake. Hawa ni watu wenye mioyo ya choyo, maono mafupi na akili mbovu. Ni bahati mbaya kuwa watu hawa wapo katika pande zote mbili; Kenya na Tanzania. Hutokea pia wachache wao sana wakawa ni watumishi wa Serikali zetu na hata wanasiasa wa pande mbili za nchi zetu. Bahati kubwa ni kuwa, sio wengi na ndiyo maana uhusiano wa nchi zetu mbili unatimiza miaka 56 sasa. Ukiwacha ule uwasili, lakini ule wa kiserikali ni miaka 56 sasa. Kwangu mimi na katika awamu yangu ya uwongozi, nitahakikisha kuwa Kenya inabaki kuwa ndugu, jirani, mshirika wa mkakati na mbia. Kenya ni nchi ya tano kwa nchi zinazoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania na ndiyo nchi ya kwanza ndani ya Afrika inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania. Nyuma ya mataifa makubwa kama Uingereza, Marekani, China na India, inakuja Kenya. Ya kwanza kituo chetu cha uwekezaji zinaonyesha ya kuwa hadi kufikia Machi, 2021, kuna miradi mingi tu ya Kenya inayotekelezwa Tanzania kama Tshs500,013,000 kutoka Kenya ambayo inatekelezwa Tanzania na kutoa ajira kwa Watanzania Tshs51,187,000 na kuchangia mapato ya kiasi cha US$1.7 billion. Sekta zinazoongoza kwa uwekezaji kutoka Kenya yaani uzalishaji viwandani, usafirishaji, kilimo, huduma, benki, ujenzi, rasilmali watu, madini, utalii na mali asili."
}