GET /api/v0.1/hansard/entries/1066962/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066962,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066962/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Tunawaalika kwa sababu Tanzania ina mambo mengi; ina rasilmali za kutosha, madini ya kutosha, ardhi kubwa na mambo mengi mengine,tunakosa mtaji. Kenya mna mtaji wa kutosha. Karibuni Tanzania. Dhamira yangu ya kuja nchini Kenya ni kuzungumza na nyinyi na kuona namna gani Watanzania wataweza kufanya vizuri zaidi nchini Kenya. Mbali na uwekezaji, ushirikiano wetu kwenye sekta ya biashara nao ni mkubwa na umeendelea kushamiri siku hadi siku. Usafirishaji wa bidhaa za Tanzania kwenda Kenya umeongezeka kutoka Tshs309.6 billioni mwaka 2017 hadi Tshs526.3 billioni mwaka 2020. Kwa upande wa Kenya nayo iliongeza kiwango cha kuuza bidhaa zake nchini Tanzania kutoka Tshs420 billioni mwaka 2007 hadi Tshs571 billion mwaka 2020. Hii inatusuta sisi viongozi na wanasiasa. Inatuonyesha kuwa wananchi wa nchi zetu mbili daima wako hatua mbele yetu. Wanafanya biashara zao kwa ubunifu mkubwa lakini sisi tunang’ang’ana na sheria na vikwazo na mambo kama hayo na tunawavuta nyuma kidogo. Ni wakati sasa wa sisi viongozi kubadilika tuwe daraja la kuunganisha watu wetu na sio tuwe vikwazo kwao. Mimi na ndugu yangu Rais Uhuru Kenyatta tumekubaliana kuweka utaratibu madhubuti wa kuzuia na kukabiliana na zile pilka pilka pale zinazotokea katika mipaka yetu wakati wa kuvusha biashara kwenda na kurudi katika nchi zetu mbili. Waheshimiwa Spika, Maseneta na Wabunge mashirikiano ya uwekezaji na biashara ni sehemu tu ya mashirikiano mazuri kati ya nchi zetu. Utalii ni eneo nyingine ambayo tunapaswa kushirikiana sana. Kama nilivyogusia ekologia zetu zinaingiliana. Hivyo hivyo, ukaribu wa vivutio vyetu vya utalii na vyenyewe vinaingiliana. Tunayo nafasi ya kunemeka pamoja ikiwa tutashirikiana katika sekta hii kuliko kushindana. Badala ya kunyang’anyana idadi ya watalii busara inatutaka tuelekeze nguvu zetu kuhamasisha mtalii aongeze idadi ya siku ambazo atazitumia nchini Kenya na Tanzania. Kwa kufanya hivyo, sote tutafaidika. Kama alivyowahi kusema Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, alisema na ninanukuu: “Tukipoteza muda mwingi kugawana kibaba - kibaba ni kipimo cha kupimia kama mchele, ngano, sembe.” Anasema tukipoteza muda mwingi kugawana hicho tutapoteza muda mzuri sana wa kuvuna kipimo kikubwa zaidi. Mashirikiano yetu yanashamirishwa pia na jitihada kubwa tunazochukua katika vita dhidi ya uhalifu, ujangili, ugaidi, madawa ya kulevya na uharamia Bahari ya Hindi na katika Ziwa la Victoria."
}