GET /api/v0.1/hansard/entries/1066963/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1066963,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066963/?format=api",
"text_counter": 59,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
"speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
"speaker": null,
"content": "Kwa vile muhalifu wa Kenya na Tanzania wana mashirikiano mazuri basi hakuna budi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama navyo vishikamane na wawe na mashirikiano mazuri ili tuweze kulinda maeneo yetu na kushinda ushirikiano wa wahalifu. Mashirikiano haya mazuri baina ya vyombo vyetu yamechangia sana kuwepo kwa utulivu na kutoa fursa kwa shule za kibiashara na uwekezaji kushamiri. Kenya ikiwa salama na sisi Tanzania tuko salama. Hali kadhalika, Tanzania ikiwa salama, Kenya nayo inakuwa salama. Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge, ujenzi wa miundo mbinu ya pamoja ni sehemu ya jitihada zetu za kuimarisha mashirikiano yetu ya kiuchumi na kimikakati. Miradi hii inajumuisha kwa uchache miradi ifuatayo: Kwanza ni ujenzi wa barabara ya lami kutoka Lamu-Mombasa kupitia Tanga-Bagamoyo hadi Dar es Salaam yenye urefu wa kilomita 454 chini ya programme ya Jumuiya ya Africa Mashariki ya kuendeleza miundo mbinu ya bara bara kwa nchi za Jumuiya ya Africa Mashariki. Katika ushorodha wa pwani - yaani coastal corridor - kwa upande wetu tuko mbioni kukamilisha ujenzi wa kipande cha Pangani-Bagamoyo na barabara za lami zenye urefu wa kilomita 124.5. Tayari tumekwisha pata fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika. Jana nilikuwa na mazungumzo na kaka yangu Uhuru naye anamalizia mazungumzo ya kupata fedha ili kazi hii ianze kwa upande wa Kenya na tukutane pale kwenye mpaka. Mradi wa pili ni barabara ya Arusha-Holili-Taveta-Voi, yenye urefu wa kilomita 260. Mradi huu ni sehemu ya mradi wa maendeleo ya barabara ya Arusha-Namanga-Athi River iliyofunguliwa rasmi mwaka wa 2002. Mradi huu unatekelezwa kwa awamu mbili. Awamu ya kwanza imeshakamilika, sasa tunajipanga kuendelea na awamu ya pili ya mradi huu. Mradi wa tatu, tunavyo vituo vya huduma vya pamoja mpakani vya Namanga: Namanga West BP na Holili Taveta West BP. Vituo hivi vimerahisisha shughuli za biashara mipakani na uvukaji wa watu. Nafurahi kuona vituo hivi vimekuwa chachu ya shughuli za kiuchumi katika maeneo ya mipaka ya mipaka yetu. Tunaendela na mchakato wa kukamilisha mifumo ya vituo vya Horohoro, Lunga Lunga na Sirari-Isebania ili navyo viweze kutoa huduma kwa wepesi na kwa ufanisi. Mradi wa nne ni wa kusafirisha umeme mkubwa wa Kw400. Kwa upande wa Tanzania mradi unahusisha ujenzi wa njia ya kusafirishia umeme kutoka Singida hadi Namanga. Ujenzi wa kituo kipya cha kuposia umeme mjini Arusha na eneo la Legumor na upanuzi wa kituo cha kuposia umeme cha Singida. Kwa upande wa Kenya, mradi huu unahusisha ujenzi wa njia ya umeme msongo wa KW400 inayojengwa kutoka kituo cha kupozia umeme cha Isinya hadi Namanga yenye urefu wa kilomita 94, inayounganishwa na njia ya umeme inayojengwa upande wa Tanzania. Benki ya Maendeleo ya Afrika pamoja na Shirika la Maendeleo la Japan, zimekubali kugharamia miradi hiyo. Mradi mwigine – Mwenyezi Mungu akijalia Inshallah - Serikali zetu mbili zitaanza kutekeleza mradi wa bomba la gesi, kuitoa gesi Dar es Salaam hadi Mombasa. Mazungumzo ya kutafuta fedha kwa ajili ya mradi huo yanaendelea. Tunatarajia yatakamilika mapema inavyowezekana."
}