GET /api/v0.1/hansard/entries/1066975/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1066975,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1066975/?format=api",
    "text_counter": 71,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mhe. Samia Suluhu Hassan",
    "speaker_title": "Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania",
    "speaker": null,
    "content": "Waheshimiwa Maspika, Maseneta na Wabunge wa Bunge la Kitaifa, hatuwezi kuuelezea uhusiano wetu vizuri bila kutambua uhusiano wa Mabunge yetu ya nchi mbili. Umekuwa ni uhusiano mzuri wa majira yote. Ninatumia fursa hii kufikisha kwenu shukrani za dhati na salamu kutoka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote kwa kuungana nasi na kutufariji katika kipindi kugumu cha msiba wa hayati mpendwa wetu Rais (Dr.) John Pombe Magufuli. Mlitufuta machozi na kutufariji sana."
}